Home news MAYELE AKUTANA KWA SIRI USIKU NA RS BERKANE…AWAMWAGIA SIRI ZA KUITUNGUA SIMBA...

MAYELE AKUTANA KWA SIRI USIKU NA RS BERKANE…AWAMWAGIA SIRI ZA KUITUNGUA SIMBA LEO…


MSHAMBULIAJI Mkongomani wa Yanga, Fiston Mayele amewapa siri timu ya RS Berkane ya kuweza kuifunga Simba watakapokutana nao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kesho Jumpili.

Siri hizo mshambuliaji huyo aliwapa Berkane baada ya kuwatembelea mara baada ya kutua nchini.

Mchezo huo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, unatarajia kuwa mkali kwani Simba watakuwa wanataka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-0 na Berkane kule Morocco.

mshambuliaji wa Berkane, Fiston Abdoul Razack amesema kuwa Mayele aliwapa mbinu hizo wakati walipokuwa wakizungumza naye na wanaamini kupitia jambo hilo watashinda mechi hiyo.

“Nimefurahi kuonana na wajina wangu Mayele ambaye kwa sasa anafanya vizuri ndani ya Yanga akiwa ndiye kinara wa mabao.

“Tumeonana na kubadilisha mawazo kuelekea mchezo wetu na Simba na ametupa vitu vingi na nina imani tutashinda,” alisema Fiston.

Kwa upande wake Kocha wa Berkane, Florent Ibenge ameweka wazi kuwa anatambua Simba ni bora zaidi wanapokuwa wanacheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini anaamini watakuwa bora zaidi kutokana na malengo yao ya kusaka ushindi.

“Malengo makubwa kwetu ni kupata ushindi, hatuna mpango wa kufikiria sare, tunataka kushinda ili kuangalia namna gani ya kwenda katika hatua inayofuata katika mechi yetu ya mwisho ya hatua hii, tunajua Simba ni wazuri zaidi wakiwa kwao lakini tumekuja kwa lengo moja kutafuta matokeo.

“Kitu kikubwa tunao baadhi ya wachezaji ambao wamecheza hapa, wanaijua vizuri Simba na hata mimi mwenyewe siyo mgeni nao. Tunatarajia kupambana muda wote,” alisema Ibenge.

SOMA NA HII  NABI: HUYU MZIZE ATAIMBWA SANA HAPA YANGA...AFUNGUKA KILICHOMPATA MAYELE...