Home Habari za michezo JESHI LA SIMBA LATIMIA….MASTAA WALIOKUWA NNJE WARUDI KIVINGINE….

JESHI LA SIMBA LATIMIA….MASTAA WALIOKUWA NNJE WARUDI KIVINGINE….

Habari za Simba

Mastaa wawili wa Simba, Moses Phiri na Henock Inonga wamerejea mazoezini  baada ya kuwa nje ya uwanja tangu Desemba mwaka jana kutokana na kuwa majeruhi.

Phiri aliumia misuli ya miguu katika mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyofanyika Desemba 21 kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba wakati Inonga alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Prisons uliofanyika Desemba 30 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezaji mwingine  ni Peter Banda ambaye nae alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu Novemba 9 mwaka jana baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars.

Phiri mwenye mabao 10 alikosa michezo minne ya Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC, Prisons, Mbeya City na Dodoma Jiji pamoja na ile ya kirafiki katika kambi ya wiki moja waliyoweka Dubai hivi karibuni wakati Inonga alikosa michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Dodoma Jiji.

Wachezaji hao wameonekana wakifanya mazoezi vizuri kwenye uwanja wa MO Simba Arena Bunju na wakiwa fiti.

Mazoezi ya timu hiyo ambayo yalianza kwa kocha Juma Mgunda kuwataka wachezaji kukimbia kwa dakika kadhaa kuzunguka uwanja ili kupasha misuli moto kabla ya baadae kugawa wachezaji katika makundi manne na kutakiwa kukimbia kwa kasi kuanzia goli la kwanza hadi la upande mwingine.

Wachezaji hao walionekana kumudu mazoezi yote hayo kwa ufasaha na kisha kuingia katika mazoezi ya kuchezea mpira.

Msemaji wa Simba, Ahmed Ally amesema wamefuraji kurejea kwa wachezaji hao kwani watakiongezea nguvu kikosi hicho kuelekea mechi ijayo ya Kombe la Azam Shirikisho dhidi ya Coastal Union itakayofanyika Jumamosi.

SOMA NA HII  SHAFFIH DAUDA AZIDI KUTIA 'KUTIA NDIMU' SAKATA LA SIMBA KUKATAA KUVAA NEMBO YA GSM..ADAI NI MSIBA...