Home Habari za michezo MRITHI WA BARBARA SIMBA HUYU HAPA….NI MTAALAMU KWELI KWELI…

MRITHI WA BARBARA SIMBA HUYU HAPA….NI MTAALAMU KWELI KWELI…

Imani Kajula CEO mpya wa Simba

Klabu ya Simba imemtangaza Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo kwa Mkataba wa miezi Sita.

Kajula anachukua nafasi iliyo wazi baada ya kuondoka kwa Aliekuwa Afisa Mtendaji, Barbara Gonzalez ambae alijiuzulu katika nafasi hiyo Desemba 10 mwaka 2022.

Kabla ya kujiunga na Simba Kajula alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu 2013.

Kajula alipata kuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyofanyika nchini mwaka 2019.

SOMA NA HII  SIMBA: TUTATANGAZA UBINGWA WA LIGI KUU BARA MAPEMA