Home Habari za michezo KAMA ZALI AISEE…TIMU ZA MBEYA ZILIVYOMRUDISHA MJINI NTIBAZONKIZA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

KAMA ZALI AISEE…TIMU ZA MBEYA ZILIVYOMRUDISHA MJINI NTIBAZONKIZA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba

Wakati mashabiki wa Simba wakichekelea na kufurahia kiwango bora cha nyota wao mpya, kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza, lakini imebainika timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zimehusika.

Ntibazonkiza alitua Simba katika kipindi cha dirisha dogo akitokea Geita Gold, ambapo amekuwa mtamu katika mechi mbili alizocheza akimpumulia kinara wa mabao, Fiston Mayele wa Yanga mwenye 15.

Nyota huyo raia wa Burundi alitamburishwa nchini na Yanga aliyoichezea msimu mmoja na kumtema kabla ya kunaswa na Geita Gold ambao walimtumia nusu msimu na Wekundu kumvuta kikosoni.

Hadi sasa Saido amefunga mabao tisa, ambapo matano ameyafunga akiwa na Simba na manne akiwa na Geita Gold na yote ameyapata kwa timu za Prisons na Mbeya City.

Saido alianza kutakata katika mechi ya kwanza akitamburishwa na Wekundu alipotupia mabao matatu ‘hati-triki’ wakati wakikandika prisons 7-1 kisha jana kuweka mawili kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya City.

Staa huyo aliingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kufunga hatitriki katika mchezo mmoja akiungana na John Bocco (Simba) aliyefunga mbili na Fiston Mayele wa Yanga na kukamilisha hatitriki nne kwenye ligi kuu hadi sasa.

Kama haitoshi mwamba huyo hakuishia kufunga tu, bali alihusika pia kwenye mabao mawili kwenye mechi hizo na kuisaidia timu yake kubaki na pointi sita na kubaki nafasi ya pili kwa pointi 47.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...AZAM FC NAO HAWAKO NYUMA AISEE...WAMNYATIA BEKI KISIKI WA YANGA....