Home Habari za michezo MASHINE MPYA YA KUTIKISA VYAVU YAPANIA KUSHUSHA UFALME WA MAYELE BONGO…

MASHINE MPYA YA KUTIKISA VYAVU YAPANIA KUSHUSHA UFALME WA MAYELE BONGO…

Habari za Yanga

Kinara wa mabao kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Fancy Kazadi anayekipiga Singida Big Stars amesema hakuja kuangalia rekodi za mastaa wengine waliopo kwenye Ligi Kuu Bara bali anataka kujitengenezea ufalme wake mwenyewe.

Kazadi amefunga mabao matano hadi sasa kwenye mechi mbili zilizopita za Kombe la Mapinduzi huku akitoka bila ya bao katika mechi moja tu kati ya tatu alizocheza.

Akizungumza baada ya kuandika rekodi ya kufunga mabao manne kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Mapinduzi wakati wakiichakaza Azam FC 4-1 katika nusu fainali juzi, Kazadi alisema anawaheshimu washambuliaji wote wanaofanya vizuri ikiwemo Fiston Mayele ambaye ni kinara wa kutupia Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 14.

“Kilichonileta SBS ni kufunga, hivyo kazi hiyo nitaifanya kila nitakapopata nafasi, lengo ni kuona timu yangu inakuwa bora hasa safu ya ushambuliaji ninayocheza, kuhusiana na vita ya ufungaji nitashindana na mimi mwenyewe kufunga,” alisema na kuongeza;

“Nafurahi kucheza kwenye timu ambayo malengo yangu yanashabihiana nayo, tulitamani kufika fainali, kwa pamoja tumepambana na kufanikisha hilo, nitaendelea kupambana hadi katika mechi za Ligi Kuu ili kuipambania timu kufikia malengo kama nilivyofanya huku.”

Kazadi alisema hii ni mara yake ya kwanza kufunga mabao manne kwenye mchezo mmoja na kwake ni furaha kwani ameisaidia timu katika mchezo muhimu ambao umewapeleka katika fainali yao ya kwanza ya michuano hiyo.

“Hat-trick nimeshawahi kufunga nikiwa Congo lakini siyo mabao manne, hii ni rekodi nyingine nimeandika nikiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi, natamani kuona ikiendelea hadi kwenye Ligi Kuu Bara, kila mchezaji ana malengo yake, kwa upande wangu natamani kuona nikifanya vizuri huku Mapinduzi na kwenye ligi ili kuongeza ushindani kwa washambuliaji waliopo.”

Kwa upande wa kocha wake, Hans van der Pluijm alisema Kazadi ni mshambuliaji mwenye uchu wa mabao, haihofii timu yoyote atakayokutana nayo kwenye fainali na anatarajia matokeo mazuri na hatimaye kutwaa taji hilo.

“Nina timu imara ambayo inapambana na kucheza mpira wa kushambulia zaidi, nafurahia hilo, sichagui nani natamani kukutana naye kwenye fainali mimi nipo tayari kukutana na timu yoyote, natambua kila timu ni bora,” alisema na kuongeza;

“Nimepata mshambuliaji bora na makini ambaye anaweza kutumia nafasi, anatengenezewa tatu anazitumia zote hivyo kazi ni kwa viungo na mawinga kumlisha mipira ifanye mambo yake.”

SOMA NA HII  KIMEUMANA SIMBA....BWALYA HATIHATI....MORRISON NA BOCCO 'OUT'...