Home Habari za michezo MATAMANIO YA MAYELE KWA YANGA HAYA HAPA… ASEMA JUU CHINI LAZIMA IWE…LASIVYO…?

MATAMANIO YA MAYELE KWA YANGA HAYA HAPA… ASEMA JUU CHINI LAZIMA IWE…LASIVYO…?

Habari za Yanga

Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Mayele amepiga hesabu zake na kuona inawezekana kubeba viatu viwili vya ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Kiatu cha kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC ambako mpaka sasa ameshafikisha mabao 15 na kiatu cha pili, ni kwenye mashindano ya Kombe la ASFC.

Mayele hajafunga bao lolote kwenye ASFC mpaka sasa na hakuwa na msimu mzuri pia mwaka jana ambapo alifunga mabao mawili tu kwenye michuano hiyo.

“Msimu uliopita nilifunga kwenye mchezo dhidi ya Mbao na lingine niliwafunga Biashara United. Mwaka huu nataka kuona kama nitaweza kufikisha idadi kubwa zaidi.

“Mchezo wetu dhidi ya Rhino Rangers ni muhimu sana kwetu kwa sababu tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu na tusonge mbele zaidi, hivyo tumejiandaa kufanya vyema kwenye mechi hiyo,” alisema Mayele.

Yanga itashuka kwenye dimba la Benjamin Mkapa kesho siku ya Jumapili, majira ya saa 1:00 jioni kupambana na Rhino Rangers kwenye mchezo wa Hatua ya 32 b Kombe la Shirikisho la Azam.

SOMA NA HII  KAZE :- SHIDA KUBWA YA YANGA NI UWEPO WA ''MABABA WAWILI'' WENYE KAULI SAWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here