Home Habari za michezo SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA…WAKILI AKATALIWA….MAREHEMU HANS POPE ATAJWA….

SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA…WAKILI AKATALIWA….MAREHEMU HANS POPE ATAJWA….

Habari za Yanga SC Leo

Wanasheria wa Feitoto wamemkataa Mwanasheria Msomi Alex Mgongolwa wakitaka aondoke katika jopo la wanasheria wanaoiwakilisha Yanga SC kwa kuwa ni mgongano wa kimaslahi wakikumbushia marehemu Zacharia Hanspope alipotolewa kwenye kesi ya Morrison kutokana na mgongano wa kimaslahi.

Hata hivyo kamati imeona hakuna haja ya kutolewa kwa mwanasheria huyo mkongwe na badala yake aendelee kuiwakilisha Yanga.

Baada ya kikao, wakili anayemsimamia Feisal Salum akiondoka katika ofisi za (TFF) na mteja wake Feisal kwenye gari, amesema …..

“Mpaka sasa hakuna mwanga kuhusu sakata la mteja wangu, sifahamu kama atarejea Yanga ama laa. Wenye kujua hilo ni (TFF)”

Alipoulizwa kama anachochote cha kuwaambia WanaYanga na kuhusu mteja wake kwamba atarejea Dubai au atabaki nchini Tanzania? ameema….;

“Sina chochote cha kuwaambia mashabiki wa Young Africans sports club.. Kwa sasa mteja wangu (Feisal Salum Abdallah) atakuwa akipatikana Zanzibar

SOMA NA HII  KUELEKEA MCHEZO WA PILI SAUZI...BARBARA KAONA ISIWE TABU..KATANGULIA YEYE MWENYEWE...KAFUNGUKA HAYA..