Home Azam FC WAKATI LEO NDIO SIKU YA MWISHO USAJILI BONGO….AZAM KUTETEMESHA JIJI.. FEI TOTO...

WAKATI LEO NDIO SIKU YA MWISHO USAJILI BONGO….AZAM KUTETEMESHA JIJI.. FEI TOTO ATAJWA..

Tetesi za Usajili Yanga

Zimesalia takribani saa kadhaa pekee kwa dirisha la usajili la mwezi Januari kufungwa katika ligi kuu Tanzania Bara.

Wakati muda ukizidi kututupa mkono ndivyo presha na hamu za mashabiki wa soka zinazidi kushika kasi kutaka kufahamu nani kasajaliwa na nani katoka kwenye klabu zetu nchini.

Kwenye tetesi za usajili inadaiwa Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, @azamfcofficial wamebakiza mchezaji mmoja pekee kama ingizo jipya dirisha hili na kinachosubiriwa ni kutambulishwa tu.

Mpaka sasa Azam FC wameshamtambulisha mlindalango Abdulai Iddrisu kutoka Ghana kwa Mkataba wa miaka miwili.

Tetesi za awali zinadai kuwa huenda Azam FC wakaisimamisha nchi pale watakapomtambuisha kiungo wa Yanga, Feisal Salum Fei toto kuwa mchezaji wao mpya.

Itakumbukwa kuwa toka mwezi disemba mwaka jana, Fei Toto alipoiandikia klabu yake ya Yanga barua ya kuvunja mkataba wake, alikuwa akihusishwa kutua Azam FC.

Chanzo chetu cha kuaminika kinadai kuwa Azam walishamalizana naye kitambo kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha kuongeza endapo pande mbili zikiafikiana.

Katika mkataba huo, Fei Toto alikubaliaa na Azam kuwa atalipwa Milion 16 kama mshahara, kupewa nyumba Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na gari ya kisasa ya kusafiria.

Mbali na hivyo, Mchezaji huyo na Azam inasadikika kuwa angelipwa Milioni 300 kama sehemu ya ada ya usajili wake, pesa ambayo alilipwa akatumia sehemu ya pesa hiyo kuilipa Yanga gharama zake za kuvunja mkataba .

Fei Toto alipangwa kutamblishwa kabla ya michauno ya mapinduzi kuanza, ambapo wakati harakati hizo zikiendela Yanga wakakimbilia TFF kukata rufaa kuomba upembuzi yakinifu wa kisheria kwenye sakata hilo.

TFF kupitia kamati ya hadhi ya wachezaji ilipitia ombi hilo, na kutoka na maadhimio ya kwamba Fei Toto ni mchezaji wa Yanga na kuipiga mkwara timu yoyote itakayotaka kumsajili bila kufuata taratibu.

Kutoka kwa maadhimio hayo, kuliifanya Azam FC kuingia ubaridi na kusitisha zoezi la kumtambulisha, huku wakienda mbali zaidi kukana kuhusika na kumtaka mchezaji huyo.

Hata hivyo, Fei Toto pamoja na timu yake ya mawakili wamekusudia kupeleka sakata hilo CAS, Huku wakiiandikia FIFA kuomba idhini ya mchezaji huyo kuichezea timu anayoitaka kwa kipindi hiki huku sakata lake likiwa linashughulikiwa CAS.

Yote kwa yote si , Azam FC wala Fei Toto mwenyewe amekiri hadharani kuwa kama wanamakubaliano ya aina yoyote,japo lolote linaweza kutokea.

SOMA NA HII  BREAKING....MASTAA SIMBA WAONDOLEWA TAIFA STARS...SABABU HIZI HAPA...