Home Habari za michezo YANGA WAFANYA KWELI KWA MUSONDA….MSHAHARA WAKE TU NI KUFRU NA NUSU…SIMBA WALIA…

YANGA WAFANYA KWELI KWA MUSONDA….MSHAHARA WAKE TU NI KUFRU NA NUSU…SIMBA WALIA…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga imemtambulisha mchezaji mpya Kennedy Musonda kutoka katika klabu ya Power Dynamos ya nchini Zambia huu unakuwa usajili wa pili wa Yanga katika dirisha dogo baada ya Mudathiri Yahya ambaye alimaliza mkataba wake na Azam Fc.

Musonda mwenye miaka 28, amesajiliwa Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea klabu ya Power Dynamo ya nchini Zambia.

Awali mchezaji huyo ambaye alikuwa anawaniwa vikali pia na Simba, klabu yake ililalamika kuwa Yanga wametumia njia isiyo halali katika kumpata.

Musonda anakuwa mchezaji wa pili kutoka Zambia kujiunga na wananchi, akitanguliwa na Lazaro Kambole ambaye nafasi yake ni finyu kwenye kikosi cha Nabi.

Inasemekana mchezaji huyo amekubali kandarasi ya miaka miwili yenye kumuhakikishia mshahara wa dola 3500 kwa mwezi sawa na karibu milioni 9 za kitanzania.

Pamoja na mshahara huo, Musonda atapewa usafiri huku makazi yake yakiwa ni kwenye kambi za Yanga kigamboni Avic Town.

Akiwa na Power Dynamo, Musonda amekuwa na kiwango kizuri kiasi cha vyombo vy habari nchini Zambia kumpa sifa kemkem ambazo zilimfanya Rais wa Yanga kutumia njia za Kimafia kumsajili akiwaacha Simba kwenye mataa.

Kusajiliwa kwa mchezaji huyo kunamaanisha kuwa sasa timu hiyo wataachana rasmi na Yacouba Sogne ambaye ameshindwa kuonyesha kiwango bora akiwa na timu hiyo kwenye mashindani ya Mapinduzi.

Ikumbukwe kuwa Msemaji wa Yanga Sc Ally Kamwe akisema kuwa wanahitaji kusajili wachezaji wawili wa kimataifa kwenye dirisha hiili dogo ambalo linatarajia kufungwa Usiku wa Januari 15, 2023.

SOMA NA HII  CARLINHOS ATAMBA KUENDELEA KUUWASHA MOTO YANGA