Home Habari za michezo YANGA WAIBUKA NA ISHU YA PSG KUWAIGA KWENYE JEZI….MADAI YAO YAKO HIVI…

YANGA WAIBUKA NA ISHU YA PSG KUWAIGA KWENYE JEZI….MADAI YAO YAKO HIVI…

Habari za Yanga

Mbunifu maarufu wa mavazi nchini Tanzania ambaye amekuwa akibuni jezi za Klabu ya Yanga kila msimu amedai kuwa klabu kubwa duniani kutoka nchini Ufaransa, PSG wameiba wazo la ubunifu wa jezi zao kutoka kwake.

Ngowi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya PSG kuingia dimbani na jezi zenye ubunifu unaofanana na jezi namba mbili (jezi ya ugenini ya Yanga) yenye rangi ya njano.

Wakati wa uzinduzi wa jezi hiyo mwanzoni mwa msimu huu, Ngowi alisema alama za mtandao (network) zilizopo katika jezi hiyo zinaonyesha muunganiko wa matawi na mashabiki wa Yanga nchi nzima na duniani kote.

Alichoandika Sheria Ngowi mbunifu wa mavazi wa klabu ya Yanga SC.

“Ninaposema mimi ni mbunifu namba moja Afrika muwe mnanielewa .. Ubunifu wangu kwa Yanga SC uko mbele ya wakati,, Haya PSG hao baada ya kufanya mimi .. Kuna mwenye swali?!” amesema Sheria Ngowi.

Katika mechi hiyo ya juzi usiku kati ya PSG iliyoongozwa na Lionel na kombaini ya Al Hilal na Al Nassr iliyoongozwa na Cristiano Ronaldo za Saudi Arabia, PSG iliibuka na ushindi wa bao 5-4.

SOMA NA HII  MAYELE ,AZIZ KI WAMFANYA KOCHA WA MAZEMBE KUSEMA HAYA KUHUSU YANGA...