Home Habari za michezo YANGA WABEBWA TENA SHIRIKISHO….CAF YAPANGUA NJAMA CHAFU ZA WATUNISI…STORI IKO HIVI..

YANGA WABEBWA TENA SHIRIKISHO….CAF YAPANGUA NJAMA CHAFU ZA WATUNISI…STORI IKO HIVI..

Tetesi za Usajili Yanga

WAKATI Yanga ikipiga hesabu kali za jinsi gani itaanza mechi yake ya kwanza ugenini ya hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kuna habari njema imepokea ambazo zimewaumiza wenyeji wao US Monastir ya Tunisia.

Yanga imebakiza siku 7 kabla ya kupaa kuelekea nchini Tunisia kukutana na Monastir lakini wenyeji wao hao walikuwa wanapambana kuwapeleka wageni wao uwanja mmoja ambao ingekuwa ngumu kutoka salama kwa wawakilishi hao wa Tanzania katika shirikisho.

Monastir baada ya kuwapiga Club Africain kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi, walijipanga kuhakikisha mchezo wao upigwe Uwanja wa Mustapha Ben Jannet.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia kurugenzi yake ya mashindano imewapiga stop! Monastir kucheza mechi dhidi ya Yanga katika uwanja huo wakiwaambia marekebisho waliyowaagiza kuyafanya hayajawaridhisha.

Haraka CAF imewataka Monastir kusaka uwanja mwingine na hesabu zao zimekosa namna zaidi ya kuwarudisha Yanga katika uwanja ambao waliweka rekodi kubwa ya kibabe dhidi ya Club Africain.

Mchezo huo una asilimia kubwa sasa utapigwa katika Uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic mjini Rades ambao Yanga iliutumia kuichapa Club Africain bao 1-0 na kutinga hatua ya makundi, Novemba 9,2022.

Ushindi huo ni wa kwanza sio kwa Yanga tu bali hakuna timu ya Tanzania iliyowahi kuondoka na ushindi katika ardhi yoyote ya Kaskazini mwa Afrika.

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ambaye ni raia wa Tunisia alisema taarifa hizo ni kitu kizuri wakati huu wakianza kupiga hesabu za kuwafuata Monastir.

Nabi alisema kwa amatokeo yao ya mwisho dhidi ya Club Africain isingekuwa taarifa njema kwao kucheza katika Uwanja wa Mustapha Ben Jannet ambapo kungekuwa na matukio mengi ya kuwaondolea utulivu.

Hata hivyo, Nabi alisema kitu kikubwa sasa ni maandalizi yao juu ya Waarabu hao kutokana na ubora wao wa kupanda tofauti na Club Africain.

“Hizi ni taarifa nzuri kwetu tulikuwa tunapiga hesabu nyingi jinsi ya kucheza Uwanja wa Mustapha Ben Jannet, wanajua tulishinda kule kungekuwa na vurugu kabla ya mchezo.

“Hatua kubwa ni sisi kujiandaa kucheza kwa ubora, watu wasidhani Monastir nkama Club Africain, Monastir wana timu bora zaidi wana mawinga wenye kasi na viungo wa kati bora.”

Yanga itacheza na Monastir Februari 12 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi huenda timu hiyo itasafiri siku sita kabla ya mchezo huo.

SOMA NA HII  KUMBE HII NDIO SIRI YA MASHABIKI WA YANGA...KUSHANGILIA KWENDA ROBO