Home Habari za michezo RASMI…CAF WAIPITISHA SIMBA KUSHIRIKI AFRICAN SUPER LEAGUE…WATAPEWA BILI 5.8…TFF NAO WATAAMBULIA ...

RASMI…CAF WAIPITISHA SIMBA KUSHIRIKI AFRICAN SUPER LEAGUE…WATAPEWA BILI 5.8…TFF NAO WATAAMBULIA BIL 2…

Habari za Simba

Baada ya tetesi za muda mrefu, Simba imepiga bao la kisigino kwa kuteuliwa kuwa timu pekee ya Tanzania itakayoshiriki mashindano ya African Super League na kwa kuanzia itavuna Dola 2.5 milioni (Sh5.8 bilioni) kwa ajili ya maandalizi yake.

Habari za uhakika ambazo ni kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) wameshateua timu nane ambazo zitashiriki mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza Afrika, huku Simba ikiwa mojawapo na tayari imeshajulishwa kuhusu hilo kwa ajili ya uthibitisho na uongozi wa Simba chini ya bodi inayoongozwa na Salim Abdallah ‘Try Again’, umeshawasha taa ya kijani kwa kuthibitisha ushiriki.

Vigogo wa kamati za mashindano na ile ya leseni za klabu wa Caf watatua nchini, Februari 14 kwa ajili ya kukutana na Simba ili kuwapa mwongozo wa namna watakavyoshiriki pamoja na ukaguzi wa kuona utayari wa wawakilishi hao.

Katika ujio huo, vigogo hao wa Caf watafanya ukaguzi wa viwanja, ambavyo Simba inatumia kwa mazoezi, uwanja ambao utatumika kwa mechi za mashindano hayo, ubora wa miundombinu kama hoteli na barabara kwa ajili ya kutumiwa na timu na wageni wengine watakaokuja kushiriki.

Maofisa hao wa Caf watakagua vitabu vya mapato na matumizi vya Simba, lakini pia namna inavyoendesha shughuli za kiutawala ili kujiridhisha kama Simba imetimiza vigezo na masharti ya kushiriki mashindano hayo.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alikiri kupata taarifa juu ya ujio wa vigogo hao wa Caf ingawa alisema watatoa taarifa kamili baada ya muda mfupi.

“Ni kweli ujumbe wa Caf utakuja kututembelea kwa ajili ya masuala ya African Super League na taarifa zaidi zitatolewa, watu wasiwe na shaka,” alisema Mangungu.

Miongoni mwa faida za mashindano hayo, ni mgawanyo wa fedha kiasi cha Dola 1 milioni (Sh2.3 bilioni ) kwa kila nchi mwanachama wa shirikisho hilo, ambalo lina jumla ya wanachama 54.

Gharama za jumla za uendeshaji mashindano hayo ni kiasi cha Dola 100 milioni (Sh233 bilioni) na bingwa atavuna kitita cha Dola 11.5 milioni (Sh35 bilioni).

Mashindano hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi 10, kuanzia Agosti hadi Mei, yakianza na timu nane

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO ...MASTAA HAWA WANNE WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC...