Habari za michezo
MANARA ALIANZISHA TENA NA TFF…AIRARUKIA KWA KUMPENDELEA MANULA …
admin
February 9, 2023
11:52 am
Haji Manara aitolea uvivu Bodi ya Ligi kuu ya NBC Tanzania bara (TPLB) kuhusu takwimu za Golikipa wa Simba SC, Aishi Manula.
Manara ameshangazwa na takwimu za clean sheets (idadi ya mechi alizocheza bila kuruhusu goli) 11.
“Pls Pls Pls acheni kucook Namba,mnaharibu sana ndugu zangu. Mnaweza kutwambia hizo Cleansheet kumi na moja kazipatia wapi na game zipi?
“Sio lazma kupika pika Statistics, bado mmehesabu hadi game aliyocheza Dakika chini ya 45, leo mmemuongezea nyingine, mnajiondolee uhalali wa kuaminika Kwa hizo data zenu.
“Mnalosahau @azamtvtz wanatuonyesha mechi zote hizo na takwimu tunazo. Hope mtafuta hii post yenu na kuweka statistics za kweli otherwise mtaonekana mmeandaa jambo kwa interest zenu.
“Nb: Au Kama vp mpeni cleansheet mia mfurahi nyie” ameandika Manara kupitia ukurasa wake Instagram,” amesema Manara.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.