Habari za Michezo
Habari za michezo

TABIA YA KUTUKANA TUKANA WATU YAMTOKEA PUANI AUSSEMS…

admin February 9, 2023 7:41 am

Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF limeanzisha uchunguzi dhidi ya kocha mkuu wa AFC Leopards Patrick Aussems kufuatia lugha ya matusi kwa mwandishi wa habari pamoja na kuwaita maofisa KPL kuwa vichekesho.

Aussems ambaye ni kocha wa zamani wa Simba ya Tanzania alisema maneno hayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya KPL dhidi ya Nzoia Sugar uliomalizika kwa sare tasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari alimuita mwandishi mmoja aliyemuuliza swali kuwa ni ‘mpuuzi’ na kuwaita maofisa wa mchezo huo kwamba wamechezesha kama vituko “wanachekesha”.

Afisa habari na masoko Pharis Kimaru alisema shitaka hilo limefika kwenye kamati ya nidhamu ya FKF.

“Tunakuja na maamuzi sawa na kitendo chake, uchunguzi ukikamilika ndani ya siku chache zijazo”, alisema Mtendaji Mkuu wa shirikisho la soka nchini humo Barry Otieno.

KISA JEZI MPYA SIMBA…MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA…’AMCHANA LIVE’ VUNJA BEI MTANDAONI… MANARA ALIANZISHA TENA NA TFF…AIRARUKIA KWA KUMPENDELEA MANULA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply