Habari za michezo

WAARABU WAPIGA HATUA MOJA MBELE KUINUNUA MAN UNITED…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin February 9, 2023 7:25 am

Miezi michache iliyopita, wamiliki wa klabu ya soka ya Manchester United kutoka Marekani wanaojulikana kama familia ya Glaziers waliweka taarifa wazi kwamba walikuwa wanatathmni hatua ya kuuza klabu hiyo.

Imebainika kwamba sasa kuna timu ya raia matajiri wa pesa za mafuta kutoka taifa la Qatar ambao wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuinunua timu hiyo.

Kulingana na jarida la Mail, Vyanzo vya habari vimefichua kundi la watu binafsi, matajiri wa juu wanaoishi katika jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, linalochochewa na uenyeji wa Qatar wa Kombe la Dunia, wameelekeza macho yao kwenye klabu wanayoiona kama ‘vito vya taji la soka’.

Watatoa ofa kwa United katika siku zijazo, kabla ya muda wa mwisho wa mwezi wa Februari uliowekwa na Glazers, na wana imani kwamba ombi lao litaondoa ushindani.

Jarida hilo lilisema kuwa matajiri hao pia wanalenga kutoa kitita kinono kwa kocha mkuu Eric Ten Hag ili kufanya usajili wa maana kwenye timu na kuimarisha ushindani wa kuwania mataji ndani ya nje ya England.

WIKI CHACHE BAADA YA KUTEMWA…KAMBOLE AWAUMBUA YANGA…ZESCO WAANZA KUMFAIDI… KUELEKEA MECHI NA WATUNISIA…NABI ‘AWASNICHI’ NDUGU ZAKE….APENYA KIMYA KIMYA MPAKA ‘CHUMBANI’..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply