Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA WAARABU..MAYELE AFICHUA JINSI MASTAA YANGA WALIVYO...

SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA WAARABU..MAYELE AFICHUA JINSI MASTAA YANGA WALIVYO NA ‘KAUBARIDI’..

Habari za Yanga

Wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wao wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Klabu ya Yanga imesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya US Monastir ya nchini humo.

Yanga SC ambao wanatupa karata yao ya kwanza leo, wamezungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi na utayari wao kuelekea katika mchezo wao dhidi ya US Monastir.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mshambuliaji kiongozi wa Yanga, Fiston Mayele raia wa Congo DR alisema wachezaji wako tayari na morali iko juu sana kwenye timu.

“Tahadhari ni kubwa sana. Monastir ni wapinzani tofauti na Club Africain. Lakini morali ya kikosi iko juu sana na ninaamini tuna imani tutafanya vyema.

“Sisi kama Wachezaji tumejiandaa vizuri na tunajua tunaenda kukutana na timu nzuri, tuko tayari na muhimu tupo hapa kupambana na tutapambana mpaka mwisho,” amesema Mayele.

SOMA NA HII  MAYELE AMPAGAWISHA NABI KAIZER...AMPIGIA SIMU MOJA