Habari za Yanga
Habari za michezo

FARHAN- ” YANGA IPO KUMZUNGUKA FEI TOTO…HATA ZAHERA ALIFANYA HIVYO”…

admin February 14, 2023 8:01 am

Wakati Yanga ikianza kampeni za Michuano ya Kimataifa pasipo kiungo wake mahiri Feisal Salum, wengi wameoneshwa kushtushwa na hali hiyo huku wakionekana kukata tamaa hasa bada ya kupata matokeo wasiyoyatarajia mbele ya US Monastr.

Sasa mchambuzi wa Soka, Farhan Kihamu amatolea ufafanuzi nafasi ya Feisal pengo la Feisal katika Kikosi cha Yanga.

“Kocha Nabi aliitengeneza Timu kupitia Feisal kwenye eneo la Kiungo, hata Mwinyi Zahera wakati yupo Yanga aliitengeneza Timu kupitia kwa Feisal na unakumbuka ndiye aliyemshusha chini acheze namba 6 ni kwa sababu Feisal ana-vission (maono) kubwa ya mchezo , umri mdogo wa maana passion (Kiu ya maafanikio) kubwa , anauwezo na ubunifu wa kufanya vitu vyote ambavyo unahitaji Kiungo afanye”

“Nabi alivyokuja hakuwa na kitu kipya zaidi ya kusema Timu itacheza lakini itaunganishwa kupitia kwa Feisal Salum, kwa sababu ni Mchezaji mwenye uwezo, hapati majeraha mara kwa mara kwa hiyo ni mradi wa muda mrefu kwa Yanga”

“Feisal anakupa kitu cha tofauti na Viungo wengine kwa sababu Feisal anapiga pasi za mbele , anapiga mashuti vyote hivi Feisal anafanya , Sasa Feisal ametoka ghafla kwenye mipango, wanapata shida sio kwamba Feisal ni bora sana kuzidi waliopo, Feisal ni pengo lakini si pengo la kwamba Feisal yeye ni pengo la kimfumo

KUELEKEA MECHI YA JUMAMOSI…WAMOROCCO WAJIBU TAMBO ZA SIMBA KIBABE… KISA KIPIGO CHA WATUNISIA….MASHABIKI YANGA ‘WAGUGUMIA NA UMBILIKOMO’ WA WACHEZAJI WAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply