Raja Twitter
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA JUMAMOSI…WAMOROCCO WAJIBU TAMBO ZA SIMBA KIBABE…

admin February 14, 2023 7:49 am

Wakati joto la mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baina ya Mnyama @simbasctanzania dhidi ya Raja Club Athletic likizidi kushika kasi, huko mitandaoni nako mambo ni moto.

Timu ya Raja Club Athletic inaonekana kama vile umewafikia ujumbe wa Klabu ya Simba wa ”Moto ni Ule ule, Kwa Mkapa hatoki Mtu.” huku ujumbe huo ukinogeshwa na picha la kibabe.

Miamba hiyo ya soka Afrika nayo imeposti ujumbe huo wa Simba ukiambatanishwa na kipande cha video kwenye akaunti yao ya kijamii ya twitter ” Habari marafiki wa Simba SC, Kiswahili changu vipi ?,”

Wekundu wa Msimbazi na Raja Club Athletic wanatarajia kukutana Benjamin Mkapa mchezo wa Ligi ya Mabinbgwa Afrika Jumamosi ya Februari 18, 2023.

KISA MAZEMBE…NABI ACHOMOA MASTAA KIKOSI CHA YANGA…CAF WAIKAZIA SIMBA DAR… FARHAN- ” YANGA IPO KUMZUNGUKA FEI TOTO…HATA ZAHERA ALIFANYA HIVYO”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply