Habari za Yanga
Habari za michezo

KIUNGO TP MAZEMBE AWAIBIA YANGA MBINU ZA USHINDI…AFUNGUKA A-Z MIKAKATI YAO ILIVYO…

admin February 18, 2023 9:44 am

Winga wa zamani wa Yanga na TP Mazembe, Chiko Ushindi Wakubanza, amesema kama Yanga watapambana zaidi na kucheza kwa moyo mmoja, basi watapata matokeo mazuri mbele ya TP Mazembe, huku akibainisha kwamba.

Ushindi ambaye aliitumikia Yanga msimu uliopita kwa mkopo akitokea TP Mazembe, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Don Bosco ya nchini DR Congo ambayo ipo chini ya TP Mazembe.

Ushindi alisema kama wachezaji wa Yanga watajituma na kucheza kwa umoja mkubwa, basi wanayo nafasi ya kupata matokeo ya ushindi mbele ya TP Mazembe, ambayo imekuwa ikipata shida ugenini katika siku za hivi karibuni tofauti na miaka ya nyuma.

“Yanga kama watapambana vizuri na TP Mazembe basi wanaweza kupata matokeo ya ushindi, ukiangalia Yanga kwa sasa wana kikosi kizuri ambacho kinaweza kupambana na kupata matokeo, ambacho wanatakiwa kukifanya Yanga kwa sasa ni kuhakikisha siku ya mchezo wanatakiwa kucheza kwa moyo mmoja, naamini watashinda.

“TP Mazembe ni timu nzuri, lakini kuna utofauti kidogo na miaka ya nyuma ambayo walikuwa wanaweza kwenda katika uwanja wowote kisha wakapata matokeo ya ushindi, lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani wamekuwa wakishinda zaidi nyumbani kuliko ugenini,” alisema mchezaji huyo.

BAADA YA KUPOTENA NA SIMBA…, MKUDE KUKAKABIDHIWA SHUGHULI ZA KANOUTE LEO.. ILE WIKIEND YA KUCHOTA MIHELA YA MERIDIANBET NDIO HII SASA…MECHI KIBAO ODDS ZA UJAZO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply