Habari za Yanga
Habari za michezo

NABI ATEGUA MTEGO WA KWANZA WA MAZEMBE …AAGIZA ULINZI MAALUMU KWA MASTAA YANGA…

admin February 18, 2023 3:47 pm

Kocha wa Yanga, Nasredinne Nabi ameanza kuishi kimkakati katika mazoezi yake kuelekea mechi dhidi ya TP Mazembe na hatua ya kwanza ameagiza ulinzi maalumu kuzuia kuangalia mazoezi ya timu yake.

Yanga inaendelea kujifua kambini Avic Town, Kigamboni inapoishi kama unataka kuwaona mastaa wa timu hiyo wakijifua mashabiki wamekuwa wakikaa nje ya uzio ulizungushiwa vyuma na kuangalia watu wanavyopambana.

Sasa juzi, Nabi aliamka na amri mpya akimuagiza mkuu wa usalama wa kambi yao kwamba hataki kuona mtu anasogea katika uzio huo wala kuangalia mazoezi hayo kwa sekunde tano.

Mmoja wa mabosi waliopo kwenye benchi la ufundi aliliambia Mwanaspoti, hataki kuona mtu ambaye ataondoka na taarifa yoyote ya jinsi ya maandalizi yao akitaka kila kitu kuwa sapraizi Jumapili.

Mbali na kuwatimua mashabiki hao pia Nabi amezuia watu wengine nje ya uongozi wa klabu kuja ndani kufuatilia mazoezi hayo akitaka kujifungia yeye na wachezaji katika maandalizi hayo.

ROBERTINHO ‘AWAJAZA PILIPILI’ MASTAA SIMBA…ASHIKILIA MSIMAMO WA KUFIKA NUSU FAINALI… BAADA YA KIPIGO CHA JANA…MO DEWJI AWACHANA MASTAA SIMBA…BANGALA ASTOPISHA JAMBO YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply