Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ akizungumzia jana maandalizi yao na mipango yao kama Timu, kuelekea mchezo wa leo wa Klabu bingwa Afrika #CAFCL dhidi ya Raja Club Athletic ya Morocco.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu, Simba ni Timu kubwa na tumejiandaa vyema ili kupata ushindi, kupambania nusu fainali na bila kipingamizi tunaweza kuwa mabingwa.
“Raja wanahistoria kubwa Afrika na Duniani kote nawajua vyema , lakini mpira ni matukio ya hapo kwa hapo (dakika 90′), mpango wangu ni kucheza vuzuri kwa sababu tunavipaji na Sisi kama Timu kubwa tuna jambo moja tu , kupata Ushindi,” amesema Robertinho
Simba na Raja zitacheza leo majira ya saa 1 kamili za jioni katika uwanja wa Mkapa, ambapo huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa kila timu ambapo kwenye mchezo wa kwanza Simba walifungwa na Horoya huku Raja akishinda mbele ya Vipers.