Habari za Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA KUICHAPA MAZEMBE…NABI AWAPA ‘MAKAVU’ WALIOKUWA WANAMSEMA KUWA NI KOCHA WA LIGI KUU PEKEE…

admin February 20, 2023 5:35 pm

Kocha Mkuu wa Yanga Nabi amewachana baadhi ya waandishi wanaodai kuwa yeye ni wa Ligi Kuu tu, lakini Kimataifa hana makali yoyote kama anavyofanya vizuri NBC.

Baada ya kuwafunga TP Mazembe, Kocha Nabi akawauliza waandishi je ushindi mnono aliopata jana ni wa Ligi Kuu?

“Si mlikuwa mnasema Nabi hawezi kimataifa? Hii mechi ya leo sio ya kimataifa,” aliwahoji waandishi Nabi.

Yanga aliibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Kufuatia ushindi huo, Yanga inakamata nafasi ya tatu kwenye kundi lao wakilingana na TP Mazembe.

Pia Jumatano, timu hiyo watashuka dimbani kukipiga na KMC kenye muendelezo wa Ligi Kuu ambapo huku wanaongoza msimamo wakifuatiwa na Simba.

BAADA YA KUFUNGWA JUZI…REFA WA KIMATAIFA AWAPA SIMBA MBINU HIZI ZA KUTINGA ROBO… ISHU YA DEREVA WA SIMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA GARI KINYUME NYUME …UKWELI UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply