Habari za Simba
Habari za michezo

MO DEWJI AIGA ALIKICHOFANYA BARBARA KWA YANGA…NAYE KAIBUKA NA HILI HADHARANI…

admin February 22, 2023 6:25 pm

Rais wa Heshima wa Simba, Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ ameibuka na kuwapongeza watani wao wa jadi, Yanga ambayo juzi waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Yanga ilipata ushindi huo katika mchezo wa pili wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Wakati Yanga wakipata ushindi huo, Simba wametoka kupoteza dhidi ya Raja Casablanca wakiwa nyumbani kwa kufungwa mabao 0-3.

Kipigo hicho cha Simba kimewafanya wawe mkiani katika msimamo wa Kundi C, wakiwa hawana pointi, huku Raja Casablanca wakiongoza wakikusanya pointi 6, Horoya (4) na Vipers (1).

Yanga wapo nafasi ya tatu katika Kundi D wakiwa na pointi tatu sawa na TP Mazembe, huku Real De Bamako wakishika mkia na pointi 1. Vinara US Monastir wenye alama nne.

SAKATA LA FEI TOTO KURUDI YANGA…INJINIA HERSI AVUNJA UKIMYA…AANIKA WANAOMRUBUNI ILI ASIRUDI KAMBINI… KAKOLANYA AWAVIMBIA MABOSI SIMBA…ATAKA MIL 100 ASAINI…AZAM FC WAMMENDEA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply