KMC vs Yanga
Habari za michezo

YANGA WAAMUA KUISHUSHIA KMC MAMBO YA TP MAZEMBE…MORRISON KAMA KAWA ‘ANAKULA BATA’…

admin February 22, 2023 11:42 am

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa leo Jumatano, katika Dimba la Mkapa.

Kaze amesema hayo jana Februari 22, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa raundi ya 22 wa ligi huku Yanga wakiwa na morali kubwa baada ya kuifunga TP Mazembe ya Congo katika mchezo wa juzi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

“Maandalizi yetu muda ulikuwa mdogo, mazoezi ni leo(jana) tu kuingia kwenye mchezo wa kesho(leo), lakini tupo sawa, ile shamra shamra za ushindi wa juzi dhidi ya TP Mazembe tumezitoa vichwani, mentally, physically na tactically tupo vizuri kwa ajili ya kukabiliana na KMC.

“Huu sio muda wa mazoezi, ilikuwa ni ku-recover tu kwa wachezaji na kurejesha utimamu kwa ajili ya mchezo husika. Tutatumia mechi mbili zilizopita (dhidi ya Monastir na Mazembe) kwa ajili ya kucheza na KMC, kujituma na kuhakikisha tunapata matokeo.

“Wachezaji tuliowatumia tangu awali ni walewale ukiachana na Morrison, Nkane na Mshery ambao wana majeruhi ya muda mrefu, wengi  wote wapo fiti. Alama tatu ni muhimu sana kuelekea mwisho wa ligi ili tuweze kutimiza malengo yetu.

“Tunakwenda kukutana na KMC, ni timu nzuri na mechi ya Yanga na KMC haijawahi kuwa nyepesi, tupo tayari, tunawaomba mashabiki wajitokeze kutusapoti, ni mechi nane za mwisho zinazokwenda kuamua mustakabali wa mafanikio ya klabu ndani ya msimu husika,”

MBRAZILI AWEKWA KWENYE MTRGO SIMBA..APEWA MECHI TATU…NABI AKABIDHIWA FAILI LA WINGA WA MAZEMBE.. WAKATI MORRISON ‘AKILA BATA’..MUSONDA AZIDI KUING’ARISHA YANGA KIMATAIFA…ACHAGULIWA CAF…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply