Home Habari za michezo FUKO LA PESA LA RAIS SAMIA LAFANYA KWELI…SIMBA WAPOKEA MAMILIONI YA PESA…

FUKO LA PESA LA RAIS SAMIA LAFANYA KWELI…SIMBA WAPOKEA MAMILIONI YA PESA…

Habari za Simba

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo Februari 26 2023 amewakabidhi Simba SC kitita cha shilingi milioni 5 ikiwa ni ahadi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ambao ni Simba na Yanga SC.

Simba jana Februari 25,2023, walifanikiwa kuwafunga goli 1-0 Vipers FC ya Uganda na kuweka kibindoni alama tatu baada ya kucheza michezo miwili ya awali kuambulia kichapo ikiwa ni hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Kwenye Kundi lao, Simba wanakamata nafasi ya tatu, juu yao wakiwa Horoya wenye pointi nne huku Raja Casablanca wakiwa vinara wa Kundi lao wakiwa na pointi 9. Vipers sasa wanakamata mkiwa wakiwa na alama moja pekee.

SOMA NA HII  HABARI YA MJINI KWA SASA NI KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET...HUKU HAKUNA KUKOSA AISEE...