Habari za Simba
Habari za michezo

KISA INONGA KUFUNGA JUZI….ONYANGO AWEKA WIVU PEMBENI….AANIKA UKWELI WA MAMBO…

admin February 28, 2023 4:44 am

BEKI wa kati wa Simba, Mkenya Joash Onyango amesema kuwa, bao lililofungwa na pacha wake, Henock Inonga dhidi ya Vipers SC ni bao lenye maana kubwa sana kwao.

Onyango amesema kuwa alichokifanya Inonga kimewapa nguvu sana na ni bao ambalo kila Mwanasimba alikuwa analihitaji na ni bao ambalo limefufua matumaini yao ya kwenda robo fainali.

Inonga alifunga bao pekee na la ushindi kwa Simba wakiwa ugenini nchini Uganda mbele ya Vipers na kuifanya timu hiyo ivune alama zake tatu za mwanzo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Onyango alisema: “Ni kitu kizuri sana kwa beki kufunga, hiyo inaonesha kuwa kila mchezaji ni muhimu na bao lake limekuwa muhimu sana kwetu na kwa Wanasimba wote.

“Nafikiri sasa tunakwenda kupambana tena kwenye mechi zijazo ili kuona kama tunaweza kwenda mbele zaidi kwenye mashindano haya.”

Simba walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Vipers kwenye mchezo uliochezwa juzi nchini Uganda na Machi 7 watacheza tena mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

KWA MAN UTD MPYA MBONA MTAKOMA AISEE…WAARABU WAPANIA KUMNUNUA MBAPPE…. YANGA KAMA SIMBA TU KIMATAIFA….WAWEKEZA NGUVU ZA DHIADA KWENYE UWANJA WA MKAPA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply