Home news ALLY KAMWE AIPA YANGA MTIHANI MZITO KWA MAZEMBE…

ALLY KAMWE AIPA YANGA MTIHANI MZITO KWA MAZEMBE…

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Afisa Habari wa timu ya Wananchi  Ali Kamwe amesema kuwa, Yanga ipo tayari kupambana kwa jasho na damu kwa silaha zote ili pointi 3 zibakie nyumbani.

Kamwe aliyasema hayo kupitia kipindi cha Sports Arena ya Wasafi FM alipokuwa akizungumzia mipango na hali ya wachezaji wa Yanga, kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAFCCL).

“Kwenye mashindano haya ni lazima kuutumia uwanja wako wa nyumbani vizuri na kupata pointi tatu, tuna mechi tano hivyo tunahitaji kushinda mechi zetu za nyumbani, Tutapambana TP Mazembe aache pointi tatu nyumbani”-Kamwe

Yanga watacheza na TP Mazembe ya DR Congo siku ya Jumapili, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Mazembe anaongoza kundi hilo kwa alama 3 na magoli matatu huku Yanga wakishika nafasi ya 3 baada ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Tunis Monastir ya Tunisia kwa mabao 2-0.

Hata Hivyo Yanga atahitaji kujitutumua na kupata matokeo ya alama 3 kwenye mchezo huo.

SOMA NA HII  SHIKA MTUTU INGIA MAWINDONI MERIDIAN BET