Home Habari za michezo FT: VIPERS 0-1 SIMBA….MNYAMAA AANZA KUUNGURUMA AFRIKA…’PAPATUPAPATU’ YAZAA MATUNDA…

FT: VIPERS 0-1 SIMBA….MNYAMAA AANZA KUUNGURUMA AFRIKA…’PAPATUPAPATU’ YAZAA MATUNDA…

Habari za Simba

WAWAKILISHI katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Timu ya Simba SC imefufua Matumaini ya kutinga Robo Fainali baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Vipers SC mchezo uliopigwa uwanja wa St.Marry’s nchini Uganda.

Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wao Henock Inonga dakika ya 20 akimalizia mpira uliopigwa na Moses Phiri.

Huo unakuwa ushindi wa Kwanza kwa Simba baada ya kupoteza mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya Raja Casablanca na Horoya AC.

Kwa matokeo hayo Simba imepanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 3, Raja anaongoza kundi akiwa na Pointi 6 huku Horoya wakiwa na Pointi 4 nafasi ya pili ambazo zitacheza baadae.

SOMA NA HII  RASMIII....OKRAH AKUNJA MIWILI YANGA....MKWANJA ATAKAOCHUMA NI KUFRU TUPU ....