Home Habari za michezo ALIYEWACHANIA MKEKA TP MAZEMBE…AJIAPIZA KURUDIA MICHEZO YAKE KWA REAL BAMAKO LEO…

ALIYEWACHANIA MKEKA TP MAZEMBE…AJIAPIZA KURUDIA MICHEZO YAKE KWA REAL BAMAKO LEO…

Habari za Yanga

Kikosi cha Yanga kimetua juzi mchana mjini Bamako, Mali tayari kwa mechi ya tatu la Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Real Bamako, huku Kennedy Musonda akitoa kauli ya kibabe akitamba kwamba kazi itaisha mapema.

Musonda aliyefunga bao moja na kuasisti kwenye mechi iliyopita dhidi ya TP Mazembe, alisema wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu.

“Tunakwenda tukiwa na utulivu mkubwa,nikweli nilipata maumivu lakini nitacheza hii mechi kama makocha wakiamua, tunataka kwenda kushinda kulekule,” alisema Musonda raia wa Zambia na kuongeza;

“Kitu ambacho tutakifanya ni kuanza kufunga mapema, tumeimarika sana baada ya kupoteza mchezo wa kwanza,unaona Kuna muunganiko mzuri kwenye timu hii ni muhimu wakati unakwenda ugenini.” “Tuna watu Bora sana kwenye eneo la kiungo na hili sio tu wale ambao walicheza mechi ya Mazembe wapo wengine lakini kikubwa pia tunavyoshirikiaana kwenye eneo letu la ushambuliaji.

Napenda sana ubora wa Fiston (Mayele) naendelea kujifunza mengi katika uzoefu wake na sina mashaka atafunga sana kwakuwa yeye ni mfungaji bora sana kwetu. Kuna wakati hata nitatakiwa kumtengeneza nafasi ili afunge na yeyote mwingine kwa kuwa kitu bora ni ushindi wa timu.”

SOMA NA HII  ODDS ZA UHAKIKA LEO ZIMELALA KWENYE MECHI HIZI....MKEKA WAKO USOME NA MERIDIANBET..