Home Habari za michezo WAZAZI WALIOMPA MTOTO WAO MCHANGA JINA LA MAYELE WAFUNGUKA…”SIWEZI KUMBADILISHA JINA HATA...

WAZAZI WALIOMPA MTOTO WAO MCHANGA JINA LA MAYELE WAFUNGUKA…”SIWEZI KUMBADILISHA JINA HATA IWEJE”…


BAADA ya kuteka hisia za wapenda soka nchini kutokana na kumuita mwanae jina la nyota wa Yanga, Fiston Mayele, shabiki wa Yanga, Victor Maguta amesema kwa kuwa hana uwezo wa kujenga sanamu la mchezaji huyo nyumbani kwake ameamua kumuita mwanae jina hilo ili kuweka kumbukumbu kwa vizazi juu ya staa huyo.

Maguta (43) ambaye ni mkazi wa Igoma jijini Mwanza na mke wake, Joyce Maguta (30) wameamua kumuita mtoto wao mwenye umri wa miezi minne jina la Fiston Mayele kama ishara ya mapenzi makubwa waliyonayo kwa mchezaji huyo raia wa DR Congo.

Maguta amesema Mayele alipojiunga na Yanga mke wake alikuwa na ujauzito wa miezi miwili hivyo kutokana na namna ambavyo Mayele amekuwa akiteka hisia za mashabiki kwa kupachika mabao kama wanandoa walikubaliana kumuita mtoto wao jina hilo.

“Nimetokea kumuita mtoto wangu Mayele kwa sababu pale mwanzoni watoto wangu nilikuwa nawaita majina ya ukoo kwahiyo nikaona huyu wa mwisho niweke mnara wa kwangu kama mpenzi mshabiki wa Yanga watoto wangu watajua kwamba baba yetu alikuwa mshabiki wa Yanga.

“Hata akihama kutoka Yanga siwezi kubadilisha jina la mwanangu hiyo ni kumbukumbu, nilipendezwa tu na uchezaji wa Mayele nikasema kwamba akizaliwa mtoto wa kiume lazima nitamuita Mayele ili nijenge sanamu kwangu kwa sababu sina uwezo wa kujenga sanamu barabarani kwahiyo nikaona nikiita jina itakuwa kumbukumbu kwamba alipita mchezaji wa Yanga ambaye alitikisa kweli,” amesema Mguta.

Mbali na mapenzi yake kwa Mayele, Mguta anasema alimhusudu sana kiungo wa Liverpool, Steven Gerald ambaye pia amempa jina hilo mwanae mwenye umri wa miaka 9.

Mtoto Mayele ni wa 10 kwa Mguta na wa nne kwa Joyce ambaye ana watoto wanne katika ndoa yake na Mguta, ambapo familia hiyo imepata nafasi alfajiri ya leo kuonana na somo wa mtoto wao Fiston Mayele katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kupiga nae picha pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.

SOMA NA HII  KAMA ULIDHANI MALENGO YA SIMBA NI MENGINE....HESABU HAYA KWA SASA.....