Home Habari za michezo KISA USHINDI KIDUCHU DHIDI YA VIPERS…’TSHABALALA’ AWAPA ZA USO MASHABIKI WANAOPONDA…

KISA USHINDI KIDUCHU DHIDI YA VIPERS…’TSHABALALA’ AWAPA ZA USO MASHABIKI WANAOPONDA…

Habari za Simba

Baada ya Simba juzi Jumamaosi kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Vipers mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ameibuka na kuanika ya moyoni.

Katika mchezo huo wa kundi C, Simba iliibuka na alama tatu kwa bao la beki wake Henock Inonga.

Baada ya mchezo huo Nahodha wa Simba Mohammed Hussein ” Tshabalala” amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kama walivyotarajia na watu wasishangae wao kuibuka na ushindi wa goli moja walilopata.

“Ilikuwa mechi ngumu na kitu pekee tulichokihitaji ni ushindi ili malengo yetu yawe hai katika champions league, Ahsanten kwa wote mliotuombea na wale washabiki wetu mliotoka Tanzania kuja kutusapoti mungu awabariki”

Simba inakatamata nafasi ya tatu katika kundi C wakiwa na alama tatu baada michezo mitatu nyuma ya vinara Raja Casablanca wenye alama 9, Horoya wakiwa na alama 4 huku Vipers wakiwa na alama 1.

SOMA NA HII  MOHAMED HUSSEIN WA SIMBA AINGIA ANGA ZA YANGA