Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU LEO…MO DEWJI KAWAPA MAAGIZO HAYA MASTAA WOTE WA...

KUELEKEA MECHI NA WAARABU LEO…MO DEWJI KAWAPA MAAGIZO HAYA MASTAA WOTE WA SIMBA..

Habari za Simba

Rais wa heshima na mwekezaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘MO’ amekutana na wachezaji wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya kutengeneza hamasa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mchezo wa pili dhidi ya Raja Casablanca utakaochezwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, bilionea Dewji amewataka wachezaji wa Simba kujituma kwa nguvu kuhakikisha kwamba timu inapata matokeo ya ushindi akiahidi kuwa yeye mwenyewe (‘MO’) atakuwepo kuhanikiza ushindi.

Dewji ametoa wito pia kwa mashabiki wa klabu ya Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa saa 1:00 usiku Leo Jumamosi ili wachezaji wapate nguvu dhidi ya mpinzani Raja Casablanca ambaye alianza vyema kampeni ya kufuzu 16 bora baada ya ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Vipers wakati Simba ikipoteza bao 1-0 dhidi ya Horoya AC.

Simba wamekuwa na rekodi ya kufanya vizuri kwenye mechi za nyumbani za kimataifa ambapo klabu kubwa zimekuwa zikipata taabu katika uwanja huo mathalani AS Vital, Al Ahly, Kaizer Chief na JS Soura.

SOMA NA HII  KUHUSU MAJEMBE MAPYA YANGA...SURE BOY ATIKISA KICHWA ..KISHA AKAFUNGUKA HAYA...AIKUMBUKA AZAM FC ...