Home Habari za michezo KUHUSU MALALAMIKO YA SPORTPESA KWA YANGA…INJINIA HERSI AWATUPIA MPIRA CAF…

KUHUSU MALALAMIKO YA SPORTPESA KWA YANGA…INJINIA HERSI AWATUPIA MPIRA CAF…

Habari za Yanga

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema mdhamini wao Mkuu ambaye ni Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa haina haki ya moja kwa moja ya kukaa kwenye vifua vya jezi za timu hiyo kama inavyoelezwa.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania na kudai kuwa, kipengele namba 15 cha mkataba wao kinawapa Yanga haki ya kumiliki eneo hilo la jezi iwapo itatokea wakashiriki mashindano ambayo SportPesa haruhusiwi kuweka nembo yake katika mashindano hayo.

Kauli hii ya Hersi inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka zogwe la kimkataba baada ya Yanga kuzindua jezi mpya zenye nembo ya Haier huku SportPesa akionyesha ukiukwaji wa mkataba wake na Yanga kwa kile alichodai kuwa hayakuwa makubaliano yao.

Msikie Hersi

“Jambo la kwanza: Wakati SportPesa wanatoa maelekezo ya SPScore (SportPesa Score), hii ni kampuni ya wapi, imesajiliwa wapi, anafanya biashara gani, ili na Yanga atakapoivaa ananufaika vipi.

Jambo la pili: Kama SportPesa alivyoielekeza Yanga aweke Kampuni ya Visit Tanzania na kuwaita siku ya pili waje kuzindua jezi. Jezi hiyo ya Visit Tanzania ni initiations za SportPesa?

Wao wanahusika vipi kwenye hilo jambo ikiwa hili jambo liko chini ya wizara? Waliihusisha wizara na wizara ikawasiliana na Yanga kufanya hilo jambo? Hakuna.

Jambo la tatu: Kama nafasi ya SportPesa kukaa kifuani ni mali ya SportPesa absolutely kwamba haiwezi kupotea. Je, ni lini walishawahi kuipeleka Yanga U-17 kampuni ya kukaa kifuani kama mbadala?

SportPesa wana haki ya kukaa kifuani ikiwa sheria yao haikinzani na sheria ya nchi, ya TFF, ya CAF ama ya FIFA.

Kipengele namba 15 cha mkataba wetu na wao kinasema itakapofikia mahali ambapo chochote katika mkataba huu kitakinzana na taratibu za nchi au mashindano tunayoshiriki, kipengele hiki kitaondolewa na hakitaathiri mkataba.

Hiyo ndiyo article inayotupa sisi haki ya kusema kwamba kwa sababu CAF wameondoa kifungu hiki na kumuondoa SportPesa kifuani, haki ile inaondolewa kwenye mkataba na inarudishwa kwenye klabu,”” amesema Eng. Hersi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTAMBULISHWA RASMI LEO...KOCHA MPYA MAN UNITED KAFUNGUKA HAYA...