Home Habari za michezo SIMBA WAKOMBA MZIGO WOTE WA YANGA KUTOKA KWA RAIS SAMIA…ISHU YOTE IKO...

SIMBA WAKOMBA MZIGO WOTE WA YANGA KUTOKA KWA RAIS SAMIA…ISHU YOTE IKO HIVI…

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amemuahidi Rais wa Taznania Samia Suluhu kwamba timu hiyo haitamuangusha kwenye mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco siku ya Jumamosi.

Rais Samia alitoa ahadi kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kwamba atanunua magoli yatakayofungwa na Simba na Yanga kwa Kila goli Tsh 5m kwenye michezo yao ya kimataifa wikiendi hii.

“Tunamshukuru sana Mh Rais Samia Saluhu kwa ahadi yake aliyoitoa tunajua zawadi hiyo itaenda kwa Simba zaidi, a itumie nafasi hii kushukuru Rais Samia kwa zawadi yake nimhakikishie hatutamuangusha”-Mwenyekiti Simba-Murtaza Mangungu

Lakini pia Mangungu aliendelea kwa kuzungumzia maaandalizi ya timu hiyo, kuelekea mchezo huo muhimu ambao Simba wanapaswa kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuangalia uwezekano wa kwenda hatua ya robo fainali.

“Maandalizi yameshafanyika na wachezaji wapo tayari kupambania ushindi wa Simba”-Mangungu

“Nisipende kukumbushia msiba kwenye maandalizi ya sharehe kwenye uwanja wa Mkapa tumezifunga timu nyingi sana, ila ni chache zimepata matokeo, tulimfunga Al Ahly, AS Vita, Nkana, kwahiyo na Raja atafungwa tu”-Mwenyekiti Murtaza Mangungu.

SOMA NA HII  GWARIDE LA UBINGWA YANGA LAWA GUMZO AFRIKA...MITANDAO MIKUBWA YALIPA UZITO...WAARABU WAPAGAWA...