Home Habari za michezo SIMBA WATULIZA PRESHA HALI YA KANOUTE…MGUNDA KAMA KAWAIDA AFANYA YAKE…

SIMBA WATULIZA PRESHA HALI YA KANOUTE…MGUNDA KAMA KAWAIDA AFANYA YAKE…

Habari za Simba

Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema Kiungo kutoka nchini Mali Sadio Kanoute anaendelea vizuri.

Kanoute alilazimika kutolewa kwa msaada wa Machela, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars, uliopigwa jana Ijumaa (Februari 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mgunda ametoa uhakika wa hali ya Kanoute, alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi (Februari 04), kuhusu maandalizi ya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Al Hilal ‘Omdurman’ ya Sudan, utakaopigwa kesho Jumapili (Februari 05), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Mgunda amesema Kiungo huyo alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo leo, lakini amesisitiza hakuumia kwa kiwango kikubwa, licha ya kutolewa kwa msaada wa Machela.

“Kanoute anaendelea vizuri na leo amekwenda kufanyiwa uangalizi zaidi, hakuumia sana lakini ninajua huenda kukawa na hofu kwa sababu alitolewa kwa msaada wa Machela.”

“Tunaamini atakuwa sawa na ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kwa michezo inayotukabili hivi karibuni.” amesema Mgunda

SOMA NA HII  KISA KUSUGULISHWA BENCHI...BIGIRIMANA AVUNJA UKIMYA YANGA...ADAI YEYE NI BORA...