Klabu ya Yanga SC imemtangaza rasmi Mtaalamu wa kuwasoma na kuwachambua Wapinzani wao ‘Video Analyst’, Khalil Ben Youssef raia wa Tunisia ikiwa ni sehemu ya kuboresha Benchi la Ufundi la Klabu hiyo.
Khalil Ben Youssef mwenye Leseni ya Ukocha Kwa Daraja B la ya CAF (CAF Coaching B License) kabla ya kutua Yanga amewahi kufanya kazi Esperance, Club Africain, Al Ahli Tripoli ya Libya pamoja na vingine vya Uarabuni.
Brain nyingine ya Maana kwenye Benchi letu la Ufundi. Khalil Ben Youssef ni Video Analyst. Mtaalam wa kufanya Uchambuzi kwenye kikosi chetu. Tutajua Perfomance za Players wetu kitaalam kabisa.
BENCHI JIPYA LA KLAB YA YANGA 2022-2023
Hii ni aada ya klabu ya Yanga kumuajiri rasmi Video Analyst , sasa Benchi la Ufundi la klab ya Yanga linakuwa na Jumla ya watu 7 kutoka mataifa 4 tofauti
1. Nasreddine Nabi – Head coach (Tunisia) 2. Cedric Kaze – Assistant coach (Burundi) 3. Milton Nienov – Goalkeepers coach (Brazil) 4. Youssef Ammar – Dk. Physiotherapist (Tunisia) 5. Moses Atutu – Team Doctor (Tanzania) 6. Prof. Helmy Gueldich – Fitness coach (Tunisia) 7. Khalil Ben Youssef – Video Analyst (Tunisia) 8. Walter Harrison – Meneja wa Timu (Tanzania) 9: Hafidh Saleh – Mtunza Vifaa (Tanzania)