Habari za Simba
Habari za michezo

ISHU YA STRAIKA WA SIMBA QUEENS KUTAMBULISHWA BESKITAS YA UTURUKI..MPANGO UKO HIVI KUMBE…

admin March 9, 2023 9:50 am

Aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba Queens Opah Clement jana Jumatano (Machi 08) alitarajiwa kutambulishwa rasmi kwa Mashabiki wa Klabu ya Beskitas inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki.

Opah aliondoka nchini juzi Jumanne (Machi 07) majira ya Alfajiri na kwenda moja kwa moja Uturuki kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo.

Opah hadi anaondoka nchini alikuwa anaitumikia Klabu ya Simba Queens na ameondoka akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Wanawake akiwa nayo tisa.

Meneja wa Simba Queens, Seleman Makanya amesema kuwa: “Opah huenda akatambulishwa leo(jana). Kwa sababu juzi aliondoka asubuhi na ilitarajiwa mchana awe ameingia.”

Opah, amejiunga na Beskitas kwa mkataba wa miaka miwili. Hii inakuwa mara ya pili kwa Opah kwenda Uturuki kucheza soka, mwaka jana alilijunga na Yikatel Kayseri kwa mkataba wa muda mfupi.

BAADA YA FEI TOTO KUTAKA KUVUNJA MKATABA YANGA…NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU JUU YAKE.. IBENGE APANIA KUMNYOFOA INONGA MSIMBAZI…MABOSI SIMBA WAKUBALI KUMWACHIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply