Habari za Simba SC
Habari za michezo

KISA MECHI YA SIMBA vs VIPERS…AHMED ALLY ‘AWANYEA’ WACHAMBUZI BONGO…”SEMENI MPAKA NUSU FAINAL”…

admin March 9, 2023 9:24 am

Baada ya Simba kufanikiwa kuibuka na alama tatu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya Makundi wakiichapa Vipers FC bao 1-0.

Wachambuzi wengi wa soka nchini wameonekana kutofurahishwa na kiwango cha Simba kinachooneshwa  katika michezo yake msimu huu huku wengi wakisema sio timu wanayoifahamu.

Sasa Meneja wa Habari na Mawasiliano , Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ambao unaonekana kuwalenga wachambuzi.

Ahmed ameandika;

“Ukisikiliza Radio unaweza kujua Simba ndo imefungwa , halafu ukisiliza tena unaweza kudhani  ndo ina point moja kwenye kundi letu, halafu ukitega sikio vizuri unaweza kuhisi kwamba  hakuna kitu kizuri tumefanya jana

Ila sisi ndo tunapenda mtukosoe hadi tufike Nusu Fainali tuliyokusudia”.

WAKATI LEO NI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI…MERIDIANBET WAFANYA KWELI ….ISHU IKO HIVI… BAADA YA FEI TOTO KUTAKA KUVUNJA MKATABA YANGA…NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU JUU YAKE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply