Home Habari za michezo PAMOJA NA MGOGORO WAKE NA YANGA….FEI TOTO ‘ALA SHAVU’ TAIFA STARS…SIMBA YATOA...

PAMOJA NA MGOGORO WAKE NA YANGA….FEI TOTO ‘ALA SHAVU’ TAIFA STARS…SIMBA YATOA WATATU TU…

Kikosi cha Taifa Stars

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Adel Amrouche ametaja kikosi cha timu hiyo kuelekea Mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi F, wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.

Kocha Amrouche ameanza kazi Stars, baada ya kusaini mkataba na TFF chini ya mwamvuli Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo itamlipa mshahara katika kipindi chote cha ajira yake.

Kocha huyo kutoka nchini Algeria atakuwa na kazi ya kuhakikisha Stars inashinda ugenini dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ Machi 24 kabla ya timu hizo kurudiana tena jijini Dar es salaam Uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 28.

Kikosi kilichotajwa na Kocha huyo ambaye ana uzoefu na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yupo Aishi Manula (Simba SC), Beno Kakolanya (Simba SC), Metacha Mnata (Young Africans), Kibwana Shomari (Young Africans), Datius Peter (Kagera Sugar), Yahya Mbegu (Ihefu FC), David Luhende (Kagera Sugar), Dickson Job (Young Africans), Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Abdallah Mfuko (Kagera Sugar), Ibrahim Baka (Young Africans), Mudathir Yahya (Young Africans), Sospeter Bajana (Azam FC) na Mzamiru Yassin (Simba SC).

Pia yupo Yusuph Kagoma (Singida BS), Ramadhani Makame (Bodrumspor – Uturuki), Abdul Suleiman (Azam FC), Edmund John (Geita Gold FC), Feisal Salum (Young Africans), Khalid Habibu (KMKM FC), Anuary Jabir (Kagera Sugar), Simon Msuva (Al-Qadsiah – Saudi Arabia) na Mbwana Samata (KRC Genk – Ubelgiji).

Wengine ni Novatus Dismas (Zulte Waregem – Ubelgiji), Alphonce Mabula (FK Spartak Subotica – Serbia), Kelvin John (KRC Genk – Ubelgiji), Ben Starkie (Basford United FC – Uingereza), Haji Mnoga (Aldershot Town – Uingereza), Ally Msengi (Swallows – Afrika Kusini) Himid Mao (Ghazl El Mahalla SC – Misri) na Said khamis (Al-Fujairah – UAE).

Hadi sasa Stars inashika nafasi ya tatu katika Msimamo wa Kundi F ikiwa ana alama 1 sawa na Uganda iliyo mkiani mwa Kundi hilo kwa vigezo vya herufi ya kwanza ya nchi hizo.

Algeria inaongoza msimamo wa Kundi hilo kwa kuwa na alama 06 ikifuatiwa na Niger yenye alama 02 baada ya kupata sare dhidi ya Tanzania na Uganda.

SOMA NA HII  MABONDIA WA NJE KINANUKA NEXT DOOR ARENA, LEO