NABI: SIWAOGOPI WAARABU...KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE...TUMEPATA SIRI ZAO
Habari za michezo

NABI SIWAOGOPI WAARABU…KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE…TUMEPATA SIRI ZAO

Marce Ben Komba March 15, 2023 5:50 am

Kocha wa Yanga, Profesa Nasreddine Nabi amesema Hawaogopi Monastir, japo waliwafunga kwao na wao wana uwezo wa kuwafunga hapa na wanaendelea kufanyia kazi Mipango kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kufuzu.

“Itakuwa mechi ngumu kwetu lakini tayari tumejua baadhi ya mipango ya wapinzani wetu hivyo tunaweza kuanzia hapo kuhakikisha tunashinda.

“Siwezi kuweka kila kitu hadharani lakini jua tunachohitaji ni ushindi tu na tuna uhakika na hilo kutokana na mechi ilivyo na vitu ambavyo tunavyo hadi sasa,” alisema Nabi ambaye anaamini kwa walivyojipanga, Yanga inatinga robo fainali.

Yanga wataikaribisha US Monastir katika mchezo wa mzunguko wa tano hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

HUYU HAPA MIKONO 60 WA AFRIKA…GOLIKIPA BORA WA MUDA WOTE AFRIKA…ATAJWA NA IFFHS SILAHA HATARI YA SIMBA YAREJEA…MSIMBAZI WAZIDI KUJIKOKI…HOROYA WATAKIMBIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply