SILAHA HATARI YA SIMBA YAREJEA...MSIMBAZI WAZIDI KUJIKOKI...HOROYA ATAKIMBIA
Habari za Simba

SILAHA HATARI YA SIMBA YAREJEA…MSIMBAZI WAZIDI KUJIKOKI…HOROYA WATAKIMBIA

Marce Ben Komba March 15, 2023 10:00 am

KIUNGO wa kazi ndani ya Simba, Hassan Dilunga amerejea kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akipambania afya yake.

Nyota huyo aliumia kwenye mazoezi wakati timu hiyo ilipokuwa kwenye maandalizi ya mechi zake za ushindani.

Taarifa iliyotolewa na WEKUNDU WA MSIMBAZI imeeleza kuwa HD amerejea ndani ya kikosi hicho baada ya kupona.

Hivi karibuni Dilunga aliweka wazi kuwa Bado hajaachana na WEKUNDU WA MSIMBAZI kwa kuwa hata suala la matibabu walikuwa wanagharamia.

Pia alibainisha kwamba licha ya kwamba hakuwepo kwenye utambulisho bado jezi yake namba 24 hakuna ambaye alipewa licha ya yeye kutokuwepo kwenye kikosi.

Kwa sasa WEKUNDU WA MSIMBAZI ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumamosi.

NABI SIWAOGOPI WAARABU…KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE…TUMEPATA SIRI ZAO KOCHA TAIFA STARS APELEKEWA MAJINI…KUINGIA NAYO KAMBINI…VIMEMO VYATUMIKA KUITA STARS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply