SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI...LOMALISA AUNGUZA KIBANDA...SIJUI ITAKUAJE?
CAF

SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI…LOMALISA AUNGUZA KIBANDA…SIJUI ITAKUAJE?

Marce Ben Komba March 17, 2023 3:40 pm

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ameonekana kumtumia zaidi Joyce Lomalisa kama beki namba tatu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kuliko Kibwana Shomari aliyeonyesha kiwango cha juu mechi za Ligi Kuu.

Kibwana amekuwa akipata nafasi mara chache lakini akionyesha kiwango cha juu.

Beki huyo alisema katika michuano hiyo inahitaji zaidi matokeo na kocha alishamwambia anamtumia Lomalisa kwa vile ana uzoefu, lakini haina maana ameshuka kiwango.

“Tunajenga Yanga kwa pamoja malengo yetu sote ni kuhakikisha tunafika mbali kwenye michuano hiyo. Lomalisa ana uzoefu mkubwa na nafurahi anapoisaidia timu, kwani kikubwa tunapata matokeo mazuri.

“Ndio maana kuna muda ananipa nafasi na nacheza ili kumuonyesha kocha napambana na nahitaji kupata uzoefu zaidi.”

Alisema pamoja na uzoefu wa Lomalisa haumfanyi aache kupambana ili kadri mechi za CAF zinavyochezwa awe mchango muhimu kikosini.

Akizungumzia mashindano hayo kwa ujumla Kibwana alisema yanamuongezea maufundi kwenye kazi yake. “Hata nisipopata nafasi kuna vitu naongeza nitafanyia kazi pale nitakapopata nafasi ya kucheza iwe kwenye ligi au mashindano hayo,” alisema.

Mchezaji yeyote anatumika kwenye mchezo kutokana na mipango ya kocha, hivyo kutokana na kucheza kwa Lomalisa ni sehemu ya mipango ya mwalimu lakini sijawahi kuchukulia kama nimeshuka kiwango.

KAMWE:- WAARABU TUMEWASOMA…TUMEWAPIGIA MAHESABU MAKALI…WATASHANGAA MPIRA BOLIBO HUYU HAPA KINARA WA KADI…MECHI 17 KADI 11…UKIKUTANA NAYE PISHA NJIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply