HOROYA AC:- HATUKUJA TANZANIA KUZURURA...MASHABIKI WA SIMBA JIANDAENI KISAIKOLOJIA
CAF

HOROYA AC:- HATUKUJA TANZANIA KUZURURA…MASHABIKI WA SIMBA JIANDAENI KISAIKOLOJIA

Marce Ben Komba March 18, 2023 2:29 pm

Nahodha wa Mabingwa wa Soka nchini Guinea Horoya AC Ocansey Mandela amesema jambo lililowaleta Tanzania ni moja tu, kushinda mchezo dhidi Simba SC, ili wajisafishie njia ya kutinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, msimu huu 2022/23.

Horoya AC itakua mgeni wa Simba SC leo Jumamosi (Machi 18) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ukiwa mchezo muhimu kwa pande zote mbili, ambazo zinahitaji ushindi.

Mandela amesema anaamini maandalizi yao kuelekea mchezo wa leo yanatosha kuishangaza Simba SC, kama ilivyowahi
kushangazwa katika michezo baadhi  ya Kimataifa kwenye Uwanja wao wa  Benjamin Mkapa.

“Hatuwezi kutoka Guinea kuja kupoteza, tumekuja kushinda ili tujisafishie njia ya kwenda Robo Fainali, na kama ambavyo timu zingine zimepata matokeo hapa basi hata sisi tutapata matokeo pia mashabiki wao wajiandae kisaikolojolia”

“Tupo kwenye Michuano hii kwa ajili ya kupambana, tumejiandaa vizuri kuikabili Simba SC ambayo tunaiheshimu sana kwa sababu ipo nyumbani kwao, tunajiamini kwa kuwa tumejiandaa kushinda hapa Dar es salaam.” Amesema Mandela

Endapo Simba SC itashinda leo Jumamosi (Machi 18) dhidi ya Horoya AC itafikisha alama 09 na kutinga moja kwa moja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kuungana na Raja

HII HAPA WIKIENDI NYINGINE YA KUBEBA MTONYO KUTOKA MERIDIANBET….ZINGATIA ODDS HIZI TU… KOCHA YANGA AMPIGIA SALUTI DIARRA…AONGOZA KWA UOKOAJI SHIRIKISHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply