FEISAL SALUM ""FEI TOTO" ATENGWA NA KIKOSI...ANAPEWA MAZOEZI PEKE YAKE
Habari za michezo

FEISAL SALUM “”FEI TOTO” ATENGWA NA KIKOSI…ANAPEWA MAZOEZI PEKE YAKE

Marce Ben Komba March 24, 2023 4:00 pm

Kiungo wa Yanga na timu ya Taifa, Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amepewa mazoezi maalumu kwa ajili ya kumuongezea fitinesi kuelekea kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda.

Stars leo itakuwa mgeni wa Uganda kwenye Uwanja wa Suez Canal, mjini Ismailia nchini Misri ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.

Kumbuka Desemba mwaka jana Fei Toto alitangaza kuvunja mkataba wake Yanga na tangu wakati huo hajacheza mechi yoyote ya mashindano zaidi ya kufanya mazoezi binafsi.

Gazeti la Championi ambalo lipo mjini hapa tangu Stars wanafika, lilimshuhudia Fei Toto akifanya mazoezi hayo na kwa mujibu wa kocha wa viungo, amesema kuwa kiungo huyo amekuwa akifanya mazoezi mara mbili zaidi ya wenzake ili kumtengenezea fitinesi kutokana na hali yake ilivyo.

Fei Toto alianza mazoezi hayo maalumu juzi Jumatano hadi jana ili kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Uganda

WAZIRI “MWANA FA:- AWAFUNGA MDOMO TFF…NDONDO CUP 2023 ITAFANYIKA KOCHA TAIFA STARS:- HAKUNA SABABU YA KUSINGIZIA…TUTAWAPA FURAHA WATANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply