Habari za Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MO DEWJI KULIA HASARA NA SIMBA….MCHAMBUZI MWINGINE AMZODOA JUMLA JUMLA…

admin March 25, 2023 5:47 pm

Wakati mahojiano ya Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, na mdhamini wa Klabu hiyo Mohammed Dwji yakizidi kuwaacha watu na maswali, baadhi ya wapenda soka nchini wameendelea kutoa maoni yao kuhusian na mahojiano hayo aliyofanya na kituo cha Global TV.

Akinukuliwa Mo alisema tangu aanze kuwekeza pesa zake ndani ya Klabu hiyo hajapata faida zaidi ya hasara.

Sasa Mchambuzi wa michezo kutoka kituo cha Wasafi FM, George Job amekuja na maoni yake kuhusiana na kauli za tajiti huyo wa Simba.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sports Arena George anasema;

“Kila mmoja anaelewa kwamba kwenye mpira kuna hasara na yeye (Mo Dewji) anajua hilo. Hamna kitu kinachonikwaza kama kila siku utuambie unapata hasara. Kila anapoibuka ni mada ya kupata hasara. Kama amechoka atoke nje ya timu.”

USAJILI WA SIMBA WASHTUA…KOCHA MPYA ASHIKILIA MAFAILI YA MASTAA HAWA KOSA KOSA ZA KIBU ZIBUA JIPYA SIMBA…MBRAZILI ASHIDWA KUMVUMILIA..AMPA MAKAVU YAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply