Home Habari za michezo JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU…LIGI YA CHAMPIONSHIP

JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU…LIGI YA CHAMPIONSHIP

JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU

Timu ya JKT Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Championship baada ya kuichapa Transit Camp bao 1-0 jana Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, JKT inafikisha pointi 56 na kuendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi saba zaidi ya Kitayosce baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Pamba SC yenye pointi 47 za mechi 22 ni ya tatu.

SOMA NA HII  BALOZI AIFAGILIA SIMBA...ATOA TAHADHARI KWA WAPINZANI.