Habari za Simba SC
Habari za Simba

RAISI WA SIMBA MO DEWJI…KILA SIKU UNALALAMIKA HASARA… KAMA UMEOCHOKA ACHIA TIMU

Marce Ben Komba March 26, 2023 4:15 pm

Wakati mahojiano ya Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, na mdhamini wa Klabu hiyo Mohammed Dewji yakizidi kuwaacha watu na maswali, baadhi ya wapenda soka nchini wameendelea kutoa maoni yao kuhusiana na mahojiano hayo aliyofanya na kituo cha Global TV.

Akinukuliwa Mo alisema tangu aanze kuwekeza pesa zake ndani ya Klabu hiyo hajapata faida zaidi ya hasara.

Sasa Mchambuzi wa michezo kutoka kituo cha Wasafi FM, George Job amekuja na maoni yake kuhusiana na kauli za tajiti huyo wa Simba.
Akizungumza kupitia kipindi cha Sports Arena George anasema;

“Kila mmoja anaelewa kwamba kwenye mpira kuna hasara na yeye (Mo Dewji) anajua hilo. Hamna kitu kinachonikwaza kama kila siku utuambie unapata hasara. Kila anapoibuka ni mada ya kupata hasara. Kama amechoka atoke nje ya timu.”

SHOMARI KAPOMBE NA MOHAMED HUSSEIN “TSHBALALA”… WAITWA KUONGEZA NGUVU TAIFA STARS KOCHA TAIFA STARS AFUNGUKA SIRI NZITO…MECHI DHIDI YA UGANDA…ILIYOWAFANYA WASHINDE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply