Home Habari za michezo KUHUSU TAARIFA YA TAIFA STARS vs UGANDA KUPIGWA USIKU SANA…UHAKIKA HUU HAPA…

KUHUSU TAARIFA YA TAIFA STARS vs UGANDA KUPIGWA USIKU SANA…UHAKIKA HUU HAPA…

Taifa Stars

Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limethibitisha taarifa za kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza kwa mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi F, kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda ‘ The Cranes’.

Miamba hiyo ya Afrika Mashariki itakutana kesho Jumanne (Machi 28), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku mchezo uliopita uliopigwa Uwanja wa Suez Canal nchini Misri ukishuhudia Tanzania ikichomoza na ushindi wa 0-1.

Afisa Habari na Mawasilino wa TFF Clofford Ndimbo amesema mchezo huo uliopangwa kuanza saa moja usiku, umesogezwa hadi saa mbili usiku, baada ya CAF kuridhia ombi waliloliwasilisha tangu juzi Jumamosi (Machi 25).

Ndimbo amesema sababu kubwa ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kutoa nafasi kwa watanzania wengi kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa, baada ya kumaliza ibada ya kufturu katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Ushindi wa Ijumaa (Machi 24) ulikuwa wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi F, kwani ilianza na sare ya 1-1 na Niger ugenini kabla ya kucharazwa mabao 2-0 nyumbani na kinara, Algeria na kesho Jumanne (Machi 28) itarudiana na The Cranes ili kufufua matumaini ya kwenda AFCON 2023 kwa mara ya tatu.

Aidha kwa upande mweingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema eneo la mzunguka katika Uwanja wa Mkapa Mashabiki wataingia bure baada ya wadau kununua tiketi zote ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa kwa Taifa Stars wanaocheza mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON2023.

“Eneo la mzunguko tayari limeshajaa, kuanzia saa 6:00 mchana milango itakuwa wazi kwahiyo mtanzania yoyote popote ulipo kuwahi kwako kufika ndio kuingia kwako. Kwenye eneo la mzunguko, kila mtanzania ana nafasi ya kuingia uwanjani kwakuwa tayari zimeshalipiwa “

” Kama tiketi zingekuwa chache tungetangaza utaratibu wa namna ya kupata lakini kwakuwa tayari zimenunuliwa zote basi milango ipo wazi kwa wote “

SOMA NA HII  UBABE WA MBAPPE KWENYE MAGOLI UNAVYOBAMBA NA MAOKOTO YA MERIDIANBET...