Home Michezo FEISAL SALUM “FEI TOTO”…MECHI NA UGANDA TUTASHINDA

FEISAL SALUM “FEI TOTO”…MECHI NA UGANDA TUTASHINDA

Fei toto Taifa Stars

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kutua nchini Misri amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maandalizi ya mechi dhidi ya Uganda kufuzu Afcon 2023.

Fei Toto akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam amesema wamejiandaa vizuri na wanaahidi ushindi kwa watanzania.

“Kweli kuna wachezaji wapya na mwalimu mpya ila Uganda tunawaheshimu ni timu nzuri ina wachezaji wazuri, ila tutaipambania Taifa Stars ili tupate matokeo,”

Ameongeza; ” Katika mechi mbili watuombee dua na tutapata matokeo kwa uwezo wake Mungu,”

Taifa Stars itacheza mechi mbili na Uganda ikianzia ugenini Misri Machi 24 na kurudiana Machi 28 jijini Dar.

SOMA NA HII  BAADA YA KUITUNGUA TENA YANGA SC...SOPU NAYE ALIAMSHA KWA DIARRA...