Home Azam FC JULIO:- AZAM FC WANIPE TIMU TUSHINDE LIGI KUU MIAKA KUMI MFULULIZO…

JULIO:- AZAM FC WANIPE TIMU TUSHINDE LIGI KUU MIAKA KUMI MFULULIZO…

Habari za Azam

Kocha Mzawa Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema haoni sababu za Klabu ya Azam FC kushindwa kutamba katika Soka la Bongo, pamoja na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara mara kwa mara.

Azam FC tangu imeanzishwa mwaka 2004, imetwaa ubingwa wa Tanzania Bara mara moja, msimu wa 2013/14 ikiipiku Young Africans iliyokuwa Bingwa msimu mmoja nyuma.

Akizungumza katika Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM , Kocha Jamhuri amesema anaamini Azam FC ni timu yenye sifa za kipekee nchini Tanzania, na imekua ikidhihirisha hilo kwa vitendo, lakini inakwama kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Azam ndio Timu iliyosajili Wachezaji wazuri tena kwa Hela nzuri sana lakini wanafeli kutokana na kutokuwa na Viongozi wa Mpira, wengi wao wanakalia majungu ukiacha Poppat”

“Ile Azam mfano nikipewa mimi niifundishe nikaenda na jopo langu la waalimu nakuahidi inabeba ubingwa miaka 10 mfululizo,” amesema Julio.

SOMA NA HII  NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA